Pages

Thursday, June 12, 2014

Ngoma Africa Band watikisa mji wa Dortmund,Ujerumani

 Si wengine bali ni bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa band aka FFU ukipenda waite viumbe wa ajabu "Anunnaki alien" au watoto wa mbwa, ambao walifanikiwa kutingisha jukwaa tena siku ya jumamosi 7 Juni 2014 mjini Dortmund,Ujerumani.katika onyesho la Challenge Festival liloandaliwa na umoja wa Wakameruni nchini Ujerumani. Wasikilize FFU Ughaibuni at www.ngoma-africa.com
 Kamanda Ras Makunja akiongoza mashambulizi
 Hapo ni supu ya mawe kwa kwenda mbele. Kamanda awapo jukwaani anacheka lakini hakuna masikhara kabisa katika gwaride
 Sehemu ya nyomi ya wadau katika onesho la FFU Ughaibuni
 Ras Makunja akikipa ishara kikosi chake wakati wa Sebene la nguvu


No comments:

Post a Comment