Pages

Thursday, June 19, 2014

Hivi ndivyo Lupita Nyongo Alivyopiga Picha za jarida la Vogue litakalotoka August 2014

Sasa tunaweza kusema rasmi kuwa Lupita Nyong’o amekuwa na mwaka mzuri katika maisha yake yote. lupita-vogue-cover
Baada ya kushinda tuzo ya Oscar kwa kuigiza kama msichana mtumwa aitwaye Patsey kwenye filamu iliyoongozwa na Steve McQueen, 12 Years a Slave na kisha kutajwa na jarida la People kama Most Beautiful Person, sasa amekava jarida maarufu la Vogue.
Lupita ataonekana kwenye jarida la August 2014 la Vogue.




Thursday, June 12, 2014

Ngoma Africa Band watikisa mji wa Dortmund,Ujerumani

 Si wengine bali ni bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa band aka FFU ukipenda waite viumbe wa ajabu "Anunnaki alien" au watoto wa mbwa, ambao walifanikiwa kutingisha jukwaa tena siku ya jumamosi 7 Juni 2014 mjini Dortmund,Ujerumani.katika onyesho la Challenge Festival liloandaliwa na umoja wa Wakameruni nchini Ujerumani. Wasikilize FFU Ughaibuni at www.ngoma-africa.com
 Kamanda Ras Makunja akiongoza mashambulizi
 Hapo ni supu ya mawe kwa kwenda mbele. Kamanda awapo jukwaani anacheka lakini hakuna masikhara kabisa katika gwaride
 Sehemu ya nyomi ya wadau katika onesho la FFU Ughaibuni
 Ras Makunja akikipa ishara kikosi chake wakati wa Sebene la nguvu


Sunday, June 1, 2014

TAZAMA PICHA 10 JINSI DIAMOND ALIVYOWEKA HISTORIA KUBWA NEW JERSEY‏ KWA SHOW KALIIII

 All Star Club Elizabeth New Jersey Diamond akikamua licha ya show kuchelewa kuanza na wapenzi wa Diamond kushikwa na jazba wakitaka aendelee lakini ikashindika kutokana na muda wa kufunga club kufika. Picha zote na Vijimambo Blog
 AJ nae akifanya yake baada ya kupewa nafasi ya ufunguzi katika show hiyo iliyofanyika New Jersey.
AJ Ubao na Dirty Hary wakishambulia jukwaa kwenye show ya kufubgua pazia iliyoanyika New Jersey na baadae Prezidaa wa Wasafi, Diamond Plutnumz kuwapagawisha mashabiki wake wa ukanda wa pwani ya mashariki.
Ni Rais wa Wasafi akishambulia jukwaa akiwa na madancer wake kwenye show ya kukata na shoka iliyofanyika New Jersey na kuvuta mashabiki kutoka kila kona ya pwani ya mashariki ambayo ni DC, PA, NJ, NY, CT, MA na kwingineko
Diamond mwanamuziki wa kizazi kipya anayekimbiza vibaya mno kwenye anga za Bongo Flava akipagawisha mashabiki wake New Jersey nchini Marekani.
Diamond na madancer wake wakijaribu kukata kiu ya mashabiki wake wa pwani ya mashariki.
 Wapenzi wa Diamond wakipagawa na show ya Diamond iliyofanyika All Star Club Elezabeth NJ.

Shabiki akidata na show ya pezidaa wa wasafi.